TUME YA TAIFA YA MIPANGO YASHIRIKI WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU
Tume ya Taifa ya Mipango imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 yanayoendelea jijini Tanga yakiongozwa na kauli mbiu imesemayo “Elimu, Ujuzi na Ubunifu njia ya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”.
Akiiwakilisha Tume kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Mipango Dkt Tausi Kida katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Ubunifu, Utafiti na Maendeleo Dkt. Evodius Kanyamyoga amesema Dira 2050 imeipambanua elimu, ujuzi na ubunifu kuwa ni miongoni mwa nguzo muhimu za mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.
Katika maadhimisho hayo Dkt. Evodius Kanyamyoga alitembelea mabanda ya taasisi mbalimbali zinaonesha bunifu na teknolojia mbalimbali katika sekta ya elimu.
Dkt Kanyamyoga amesema kuwa, kama ambavyo kauli mbinu ya maadhimisho hayo inavyojieleza, Dira 2050 inalenga kujenga Tanzania yenye ustawi, inayojitegemea na yenye uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa, teknolojia na uwezo wa wananchi wake, hivyo imeweka msisitizo katika mfumo wa elimu unaoendeshwa na teknolojia, ukuzaji wa STEM na ujuzi wa kidijitali.