Idara ya Mipango na Bajeti
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma bora za mipango, bajeti, tafiti, uvumbuzi na utoaji wa taarifa za utendaji.
Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kufanya kazi za mpango mkakati wa Tume, ikiwa ni pamoja na kuandaa Mipango Mkakati, Mipango ya Mwaka, Bajeti na miradi ya maendeleo.
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango mikakati ya muda wa kati, bajeti, mipango kazi na miradi ya maendeleo.
- Kufanya tathmini za mara kwa mara za utendaji kazi na kuandaa taarifa.
- Kuandaa Hotuba ya Bajeti ya Tume.
- Kuhifadhi takwimu za Tume.
- Kupanga na kupitia miradi ya maendeleo.
- Kuratibu masuala ya Bunge.
- Kuratibu shughuli za tafiti na ubunifu katika Tume.
- Kufanya utafiti wa Huduma zinazotolewa na Tume.
- Kukusanya, kupitia, na kuchanganua data, takwimu, na taarifa za shughuli za Tume.
- Kuanzisha mpango mkakati na mchakato wa bajeti ya Tume.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:
- Sehemu ya Mipango na Bajeti.
- Sehemu ya Tafiti na Ubunifu.