Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma za TEHAMA kwa Tume.
Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuandaa mifumo ya ufuatiliaji na utoaji taarifa.
- Kuwezesha matumzi ya TEHAMA katika utendaji kazi.
- Kuanzisha na kusimamia miundombinu ya mtandao wa mawasiliano ya Tume.
- Kusimamia na kuhuisha tovuti ya Tume.
- Kutoa huduma za kiufundi za TEHAMA kwa Tume.
- Kusanifu na kusimamia usalama wa mfumo.
- Kuwezesha kufanyika kwa shughuli za Serikali mtandao na Biashara ya kielektroniki.
- Kufanya tafiti na kupendekeza maeneo ya kutumia TEHAMA kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma katika Tume;
Kitengo hiki kitaongozwa na Meneja.