Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

Utangulizi

Serikali ilianzisha Tume ya Taifa ya Mipango mwaka 2023 kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Mipango, Sura 127. Lengo ni kuwezesha kuratibu mipango ya maendeleo ya taifa.Tume ya Taifa ya Mipango ipo chini ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ikiwa ni chombo cha juu cha ushauri kwa Serikali kuhusu masuala ya mipango ya maendelo na usimamizi wa uchumi. 

Pamoja na majukumu mengine, Tume ya Taifa ya Mipango itakuwa ina jukumu la kupanga mipango ya maendeleo ya taifa kwa muda mrefu, wa kati na mfupi. Vilevile, Tume hii ina jukuma la kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ikiwemo miradi ya kielelezo na kimkakati kwa ustawi wa maendeleo ya taifa. Aidha, Tume ina jukumu la kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo ambayo huzingatiwa katika mipango ya maendeleo ya Taifa.