Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, amewafuturisha watumishi wa Tume hiyo na kuwatakia heri ya Mfungo wa Ramadhani pamoja na sikukuu njema ya Idd. Hafla hiyo, iliyofanyika tarehe 27 Machi 2025 jijini Dodoma, ililenga kudumisha mshikamano na mahusiano mazuri miongoni mwa watumishi.
Katibu Mtendaji mpya wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, akabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Kaimu Katibu Mtendaji Dkt. Mursali Ally Milanzi, Machi 10, 2025 katika ofisi zilizopo Jengo la Kambarage Jijini Dodoma.
Tume ya Mipango yajadili Modeli ya Uchumi Jumla na Mpango Elekezi wa Dira ya Taifa 2050
Dodoma, Machi 11, 2025, Ikiwa mchakato wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uko kwenye hatua za kiserikali, wataalamu kutoka sekta mbalimbali wamekutana na kufanya kikao kazi chenye lengo la kuendelea kuweka misingi thabiti ya maendeleo ya muda mrefu kwa kujadili Modeli ya Uchumi Jumla na Mpango Elekezi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mheshimiwa Majaliwa aliimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Kitila Mkumbo, Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili aipeleke kwenye Baraza la Mawaziri na hatimaye Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kutungiwa sheria.

Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Mipango limefanya kikao cha pili, Machi 20, 2025, Jijini Dodoma, Kikao hicho kimeongozwa na Dkt. Fred Msemwa Katibu Mtendaji wa Tume na kuhudhuriwa na Wawakilishi kutoka katika Idara mbalimbali Pamoja na wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE Taifa, Kikao Kilipokea na kujadili utekelezaji wa Bajeti ya 2024/25 na mapendekezo ya Bajeti ya 2025/26 kwa ufanisi wa taasisi.
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Mipango wamepatiwa mafunzo maalumu kuhusu maadili, ushirikiano, nidhamu, na afya ya akili ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango. Mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Idara ya Rasilimali Watu, yamefanyika Dodoma tarehe 30 Januari 2025.

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Mipango na Timu ya Uandishi wa Dira ya 2050 walikutana jijini Arusha tarehe 25 Januari 2025, kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo. Wajumbe walisisitiza nafasi ya kipekee ya kijiografia ya Tanzania na fursa ya kuwa na uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050.
Maafisa wa Tume ya Mipango wamehitimu mafunzo ya siku mbili kuhusu uandaaji wa nyaraka za Baraza la Mawaziri, yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 24 hadi 26 Januari 2025. Mafunzo hayo, yaliyoendeshwa na Secretarieti ya Baraza la Mawaziri, yalilenga kuimarisha ujuzi wao katika kuandaa nyaraka rasmi, kuchambua sera, na kuandaa mikakati madhubuti ya kusaidia vipaumbele vya maendeleo ya Taifa. Hatua hii ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuimarisha mchakato wa utungaji sera na usimamizi wa serikali.