Kitengo cha Fedha na Uhasibu
Lengo
Kutoa huduma bora za usimamizi wa fedha na uhasibu.
Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuandaa Taarifa za Fedha za Robo Mwaka, Nusu Mwaka na Mwaka.
- Kukagua Vocha za Malipo na nyaraka zinazoambatana nazo ili kuzingatia Sheria za Usimamizi wa Fedha.
- Kuratibu na kujibu hoja za ukaguzi zinazoibuliwa.
- Kushughulikia malipo ya fedha taslimu na kutunza nyaraka za fedha.
- Kuandaa malipo ya mishahara na kuhakikisha makato yote ya kisheria yanatumwa kwa wakati kama inavyoelekezwa.
- Kuandaa, kufanya malipo na kufuatilia matumizi.
Kitengo hiki kitaongozwa na Mhasibu Mkuu.