Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango (NPC)

Kitengo cha Huduma za Sheria

Lengo

Kutoa huduma ya ushauri wa kisheria kwa Tume

Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kutoa msaada wa ushauri wa kisheria kwa Tume.
  2. Kuratibu na kusimamia utoaji wa huduma za kisheria wakati wa kuandaa na kupitia sheria.
  3. Kuandaa na kupitia hati za kisheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  4. Kutoa uelewa wa masuala ya sheria.
  5. Kutunza nyaraka zote za kisheria zaTume.

Kitengo hiki kitaongozwa na Meneja.