Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango (PC)

Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini

Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:

  1. Kutoa maeneo wakati wa kuandaa mipango na shughuli za programu kwa Tume.
  2. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mipango ya Mwaka na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Tume.
  3. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Maeneo Muhimu ya Matokeo ya Kitaifa (NKRA) yaTume.
  4. Kuwezesha ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi mbalimbali  kwa kuandaa  nyenzo na violezo vya ripoti kulingana na Viashirio Muhimu vya Utendaji.
  5. Kufanya tathmini za haraka za mipango ya Tume ili kufanya uamuzi sahihi kuhusu uboreshaji wa programu/mradi na maendeleo kusudi kufikia malengo ya Tume.
  6. Kufanya tathmini za matokeo ya mafanikio ya Tume dhidi ya Viashirio muhimu vya Utendaji vilivyowekwa.
  7. Kuimarisha uwezo wa ndani wa Tume wa M&E kupitia mafunzo na na kukuza uelewa.
  8. Kuandaa mfumo wa M&E wa Tume ikihusisha kuandaa na kutekeleza mwongozo wa M&E.
  9. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya tathmini ya ndani na nje.

Kitengo hiki kitaongozwa na Meneja