Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma za habari, mawasiliano na kuzungumza na umma na vyombo vya habari.
Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano wa Tume.
- Kufanya uchanganuzi wa wadau na kuchunguza ujumbe.
- Kutafiti masuala yanayoibuka kutokana na utekelezaji wa mipango ya kati na ya muda mrefu na kuandaa majibu.
- Kuwezesha ushirikishwaji wa umma katika programu za Tume.
- Kuongeza uelewa wa umma kuhusu majukumu na shughuli za Tume.
- Kuratibu mikutano ya waandishi wa habari na Tume.
- Kuratibu na kuchangia maudhui ya tovuti ya Tume.
- Kuratibu maandalizi na utayarishaji wa makala na majarida ya Ofisi.
- Kuwa kiunganishi kati ya Tume na Taasisi zingine za Serikali na umma kwa ujumla.
- Kuandaa na kusambaza taarifa kwa umma kuhusu sera, programu na mageuzi yanayofanywa na Tume.
- Kufanya ufuatiliaji na uchanganuzi wa Vyombo vya Habari.
- Kusimamia na kuhuisha Tovuti ya Tume.
- Kuratibu na kusimamia ushiriki wa Tume katika Maonyesho ya Kitaifa na Kimataifa.
Kitengo hiki kitaongozwa na Meneja.