Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

NPC: Muifanye Tanzania Taifa la Ujasiriamali
26 Aug, 2025
NPC: Muifanye Tanzania Taifa la Ujasiriamali

NPC: Muifanye Tanzania Taifa la Ujasiriamali 

Mashirika ya Umma (SOEs)yameaswa kuwa sehemu ya kuibadilisha nchi kuelekea kwenye Taifa la ujasiriamali ikiwa ni njia ya kutekeleza DIRA 2050.
Mwito huo uliyolewa jana (26.8.
2025) na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Dkt. Fred Msemwa,  Arusha.
Dkt Msemwa alikuwa akiwasilisha wasilisho la utekelezaji wa  DIRA 2050 katika kikao kazi cha tatu cha mwaka kwa wenyeviti wa Bodi na Watendaji wa mashirika ya umma katika mkutano uliohusisha wajumbe 650, ukiwa umeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Dkt. Msemwa alisema kuwa SOEs wana mchango.mkubwa sana katika kubadilisha Taifa kuwa la ujasiriamali katika kutekeleza DIRA 2050 lenye  shabaha ya kuwa na uchumi wa dola za Marekani trilioni moja ifikapo 2050.

Aliwambia washiriki kuwa kwa bahati mbaya neno ujasiriamali limekuwa likitumika kihasi, hivyo kuwafanya wengi wasijihusishe na ujasiliamali kwa kuwa wengi wanahusisha na uchuuzi.

"Mara zote tumetoa tafsiri hasi juu ya ujasiriamali, lakini ukweli ni kwamba ujasiriamali ni tofauti na uchuuzi, na kimsingi ujasiriamali unahushisha kuangalia hasara mtu anaweza kupata tofauti na mchuuzi ," alisema Dkt. Msemwa akiongeza: "Kinachohitajika ni sisi kubadili fikra zetu ili kubadilisha mashirika yawe ya kijasiriamali kuleta faida."
Aliongeza kuwa Tanzania bado haijafikia  uchumi wa soko (market economy), ambapo SOEs wanamchango mkubwa kufikia huko.
Akiwasilisha suala la utayarishaji wa Mpango Mkakati kwa SOEs alisema  NPC kwa sasa inatayarisha mwongozo wa jinsi ya kuandaa Mpango huo, hususani kwenye masuala ya Shabaha.

Dkt. Msemwa alisema kwa sasa Pato la Taifa lina thamani ya dola za Marekani bilioni 85, ambapo kufikia uchumi wa thamani ya dola triloni moja, inabidi ifanyike kazi kubwa kwani ni nogezeko mara 10.

Kwa ujumla aliwaasa washiriki kusaidia juhudi katika kuelimisha umma juu ya DIRA 2050 ili kila Mtanzan8a aweze kuelewa kilichomo kwenye DIRA 2050 na malengo yake.