Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma za usimamizi wa rasilimali watu na kiutawala kwa Tume.
Idara hii itatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kutafsiri Sheria ya Utumishi wa Umma, Kanuni za Utumishi wa Umma na Sheria zingine za kazi.
- Kusimamia utekelezaji wa shughuli za kuhamasisha maadili kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuzuia rushwa.
- Kusimamia utekelezaji wa shughuli kama vile kuajiri, uteuzi, semina elekezi, mafunzo, upandishaji vyeo, nidhamu, kuhakikisha wafanyakazi hawaondoki au kuacha kazi, motisha, kusimamia utendaji na ustawi wa wafanyakazi kwa jumla.
- Kuhakikisha matumizi na usimamizi wa rasilimali watu ulio bora na wenye ufanisi.
- Kuratibu masuala ya Baraza la Wafanyakazi na Vyama vya Wafanyakazi.
- Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa sera, utaratibu na miongozo madhubuti ya kuajiri, mafunzo, kuhakikisha wafanyakazi hawaondoki au kuacha kazi, upandishaji vyeo na kusimamia utendaji kazi.
- Kufanya ukaguzi wa rasilimali watu, mahitaji na ujuzi unaotakiwa.
- Kutoa huduma za usajili, usimamizi na utarishi; na kusimamia kumbukumbu za Ofisi.
- Kushughulikia masuala ya itifaki.
- Kuwezesha utoaji wa huduma za usalama, usafiri na mahitaji ya jumla.
- Kuwezesha matengenezo ya vifaa vya Ofisi, majengo na eneo la ofisi.
- Kuratibu utekelezaji wa shughuli za kuhamasisha maadili kwa wafanyakazi.
- Kuratibu utekelezaji wa masuala uanuwai.
- Kuratibu utekelezaji wa Ushiriki wa Sekta Binafsi, uboreshaji wa Utendaji Kazi na Mkataba wa Huduma kwa Wateja.
Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:
- Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu; na
- Sehemu ya Utawala.