DIRA NA DHIMA
DIRA
Kuwa kitovu cha mipango yenye ufanisi katika usimamizi wa uchumi jumuishi na ustawi wa jamii.
DHIMA
Kutumia takwimu na matokeo ya utafiti kwa ubunifu ili kuleta mabadiliko yenye tija kwenye ukuaji wa uchumi jumuishi.
MAADILI YA MSINGI
Tume ya Taifa ya Mipango inaongozwa na maadili ya msingi sita (6) katika utendaji kazi ambayo ni:
MAADILI YA MSINGI |
MAELEZO |
Ushirikiano |
Tunathamini juhudi za pamoja na shirikishi ili kufikia lengo moja na kuwaridhisha wadau wetu. |
Uadilifu |
Tunafanya uamuzi wa kuwajibika kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma, utu na uaminifu |
Ubunifu |
Tunahimiza ubunifu na mabadiliko ya mtazamo katika utoaji wa huduma |
Uwajibikiaji |
Tunajitolea kuchukua jukumu na umiliki wa vitendo/hatua za mtu binafsi au timu kwa njia ya uwazi |
Bidii |
Tunazingatia matokeo yenye kuleta mageuzi, uthabiti, sahihi na kutumia mbinu bora. |
Ujumuishaji |
Tumejitolea kuzingatia na kudumisha kanuni za usawa na haki. |