Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Yawasilishwa Bungeni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo (katikati), akiwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa (kulia), pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Tausi Kida, wakionyesha Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 mara baada ya kuwasilishwa rasmi mezani Bungeni leo, tarehe 26 Juni 2025, jijini Dodoma. Rasimu hiyo imewasilishwa Bungeni kufuatia kukamilika kwa mchakato wa ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi, kupitia vikao na mijadala mbalimbali na makundi ya kijamii, wadau wa maendeleo, pamoja na wataalamu kutoka nyanja tofauti. Aidha, Rasimu hiyo ilijadiliwa na kuridhiwa na Baraza la Mawaziri kabla ya kuwasilishwa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zaidi za kutungwa kuwa Sheria. Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inalenga kutoa mwelekeo wa maendeleo ya muda mrefu kwa taifa, na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 17 Julai 2025 na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna Taarifa kwa sasa