Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

Dkt. Msemwa wa Tume ya Mipango Akutana na Mfanyabiashara Maarufu Said Salim Bakhresa
05 Jun, 2025
Dkt. Msemwa wa Tume ya Mipango Akutana na Mfanyabiashara Maarufu Said Salim Bakhresa

Dar es Salaam, Juni 4, 2025

Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, leo amefanya ziara rasmi katika Makao Makuu ya Makampuni ya Bakhresa jijini Dar es Salaam na kukutana na mfanyabiashara mashuhuri barani Afrika, Bw. Said Salim Bakhresa.

Katika ziara hiyo walifanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali katika kuunga mkono mipango ya maendeleo ya taifa, ikiwemo uwekezaji katika sekta za viwanda, kilimo, na huduma. Dkt. Msemwa alielezea dhamira ya Tume ya kushirikisha wadau wakuu wa sekta binafsi ili kuunda mikakati jumuishi inayolingana na mahitaji ya soko na uchumi wa nchi.

Dkt. Msemwa amepongeza mchango Bw. Bakhresa kuwa ni wa kimkakati na wakuimarisha uchumi wa Tanzania kupitia uwekezaji wa moja kwa moja, uundaji wa ajira, na uvumbuzi wa kiuchumi. Alisisitiza kuwa ushirikiano huu ni muhimu katika kufanikisha malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kukuza uchumi endelevu na jumuishi.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Tume ya Taifa ya Mipango za kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kuhakikisha mipango ya kitaifa inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta tija kwa Wanatanzania.

#SektaBinafsi
#UjasiriamaliTanzania
#MaendeleoEndelevu