MCHANGO WA TUME YA TAIFA YA MIPANGO WATAMBULIWA WARSHA YA UTAFITI
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya REPOA kufuatia ushirikiano baina ya taasisi hizo katika utekelezaji wa maandalizi ya Warsha ya 29 ya Utafiti ya mwaka iliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa mwezi Mei, 2026.
Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Dkt. Tausi Kida na Naibu wake, Dkt. Blandina Kilama, ikiashiria mafanikio ya Warsha hiyo kwa maendeleo ya Watanzania kwa kuwa ilikuwa kiungo muhimu kilichowakutanisha watafiti na watunga sera ili kuangalia fursa zilizojificha kwenye Mito, Maziwa na Bahari (Uchumi wa Buluu).
Lengo kuu lilikuwa ni kuona jinsi rasilimali za bahari na maziwa zinavyoweza kutengeneza ajira na kuleta maendeleo yatakayomfikia kila mwananchi kuanzia mvuvi mdogo hadi mfanyabiashara mkubwa bila kuharibu ikolojia ya mazingira.