Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

Rais Samia aagiza Miradi iendane na Malengo ya Kitaifa, asisitiza umuhimu wa Tume ya Taifa ya Mipango katika usimamizi wa Dira 2050
27 May, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Samia Suluhu Hassan ameiagiza Tume ya Taifa ya Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Mipango na uwekezaji, kuhakikisha kuwa mipango na miradi ya kisekta inayotekelezwa nchini inafungamanishwa na malengo ya Kitaifa.

Rais Samia pia ameielekeza Tume hiyo kusimamia kikamilifu miradi yote mikubwa inayotekelezwa nchini.

"Watanzania wana imani kubwa na Tume hii na ninyi mmeingia kwenye kipindi muhimu ambapo Waziri anawaongoza kwenye uandikaji wa dira ya miaka 25 ijayo ya Taifa hili. Waziri ameongoza vyema uandishi wa Dira na ipo hatua za mwisho, utekelezaji utawategemea ninyi kwahiyo naomba mwende mkasimame vyema. Ni kipindi kizito na kigumu ambacho mmeingia lakini ni imani yangu kwamba mnaweza kufanya vizuri." amesema Rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Samia Suluhu Hassan ameiagiza Tume ya Taifa ya Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Mipango na uwekezaji, kuhakikisha kuwa mipango na miradi ya kisekta inayotekelezwa nchini inafungamanishwa na malengo ya Kitaifa.

Rais Samia pia ameielekeza Tume kusimamia kikamilitu miradi yote mikubwa inayotekelezwa nchini.

Katika maelezo yake, Dkt. Samia ameonesha kuwa na imani kubwa na Tume ya Taifa ya Mipango inayoongozwa na Katibu Mtendaji Dkt. Fredy Matola Msemwa, akibainisha kuwa watanzania pia wana matumaini na imani kubwa na Tume hiyo katika uratibu na usimamizi wa mipango mbalimbali ya Kitaifa, akihimiza pia kujiandaa katika ukamilishaji na usimamizi wa utekelezaji wa Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Rais Samia amebainisha hayo leo Jumamosi Mei 24, 2025, Ikutu Jijini Dar Es salaam wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni akiwemo Dkt. Blandina Kilama, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango anayeshughulikia Biashara na Ubunifu.