Tume ya Taifa ya Mipango ni nini ?
Tume ya Taifa ya Mipango (NPC) ilianzishwa mwaka 2023 kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Mipango, Sura 127. Lengo ni kuwezesha kuratibu mipango ya maendeleo ya Taifa. Tume ya Taifa ya Mipango ipo chini ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ikiwa ni chombo cha juu cha ushauri kwa Serikali kuhusu masuala ya mipango ya maendelo na usimamizi wa uchumi.
Pamoja na majukumu mengine, NPC ina jukumu la kupanga mipango ya maendeleo ya Taifa kwa muda mrefu, wa kati na mfupi. Vilevile, NPC ina jukuma la kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ikiwemo miradi ya kielelezo na kimkakati kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa. Aidha, NPC ina jukumu la kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo ambayo huzingatiwa katika mipango ya maendeleo ya Taifa.