Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

TUME YA TAIFA YA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE (Ufuatiliaji na Tathmini)
04 Nov, 2026
TUME YA TAIFA YA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE (Ufuatiliaji na Tathmini)

TUME YA TAIFA YA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE (Ufuatiliaji na Tathmini)

Tume ya Taifa ya Mipango imewasilisha mipango ya kitaifa, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na nyenzo za utekelezaji wake, mbele ya Kamati mpya ya Kudumu ya Bunge ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa, kwa lengo la kujenga uelewa wa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya Taifa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais ( Mipango) na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi M. Kida, aliwafahamisha wajumbe kuhusu majukumu ya kisheria ya Tume, ambayo yanaweka msingi wa maandalizi na uratibu wa mipango ya kitaifa.

Aidha, ameeleza kwa kina kuhusu, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Muda Mrefu  2026/27 -2050/51(Long-Term Perspective Plan) na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP IV) na majukumu ya kisheria ya Tume katika kuandaa mipango ya maendeleo ya Taifa.

Kuanzishwa kwa kamati hiyo, inayongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Daniel Baran Sillo, na inaundwa na wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutaongeza msukumo katika kuimarisha usimamizi na tathmini ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo hususan utekelezaji wa Dira 2050.


Katika kikao hicho, Dkt. Kida aliambatana na Naibu Katibu Watendaji wa Tume, Dkt. Mursari Milanzi anayeshughulikia Mipango Kitaifa, Dkt. Blandina Kilama anayeshughulikia Biashara na Ubunifu, pamoja na Bw. Sosthenes Kewe anayesimamia Menejiment ya Utendaji na Tathimi.

Wasilisho hilo linalenga kuimarisha uelewa wa pamoja kati ya Tume na Bunge kuhusu mipango ya kitaifa na nyenzo zake za utekelezaji, ili kusaidia usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya Taifa.