Dkt. Fred Msemwa, amekabidhiwa rasmi ofisi. Tume ya Taifa ya Mipango
26 Mar, 2025

Katibu Mtendaji mpya wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Kaimu Katibu Mtendaji Dkt. Mursali Ally Milanzi leo Machi 10, 2025 katika ofisi zilizopo Jengo la Kambarage Jijini Dodoma. Baada ya makabidhiano hayo Dkt. Msemwa alifanya mkutano na wajumbe wa menejimenti wa Tume, ambapo alisisitiza umuhimu wa kila mtumishi kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia viwango vya juu ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Tume unafanikiwa kwa ufanisi na kwa wakati.
Vile vile Katibu amekutana na wote wa Tume, nakuwataka kuwa na ari mpya katika utendaji wao na kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha mipango ya maendeleo ya nchi inatekelezwa kwa ufanisi.