KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPITISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26 kwa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, makadirio hayo yamepitishwa leo tarehe 22 Machi, 2024 Bungeni Mkoani Dodoma.
Kamati hiyo imepitisha makadirio ya fungu namba 011 kwa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji , na kifungu namba 066 - Tume Taifa ya Mipango na Fungu 007 - Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Awali akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji ya mwaka 2024/25 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.) amesema kuwa Ofisi yake imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki ya upatikanaji wa huduma kwa wawekezaji na wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuunganisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZA), ili kuunda taasisi moja ya uwekezaji itakayosimamia masuala ya uwekezaji nchini.
Mhe. Prof. Mkumbo amesema Sheria inayoanzisha Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority – TISEZA) ambayo itatekeleza majukumu ya TIC na EPZA. Huu, ni utekelezaji wa maamuzi ya Serikali ya mwaka 2023 yanayolenga kuimarisha ufanisi wa shughuli za uwekezaji nchini.
Mhe. Prof. Mkumbo ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikiboresha mazingira ya uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ardhi ya uwekezaji inatengwa kwa ajili ya uanzishwaji wa miradi ya uwekezaji mahsusi katika sekta za kimkakati.
Mhe. Prof. Mkumbo ameongeza kuwa Serikali imewezesha kujenga mifumo ya kutoa huduma kwa njia ya mtandao ili kuwezesha wawekezaji na wafanyabiashara popote walipo wapate huduma kwa urahisi. Aidha, amesema Serikali imewezesha kujenga mifumo ya kutoa huduma kwa njia ya mtandao, ili wawekezaji na wafanyabiashara wapate huduma kwa urahisi popote walipo. Taasisi za BRELA, OR-TAMISEMI, TBS, TIC, TMA, na TRA zimerahisisha utoaji wa huduma zinazohusu usajili wa kampuni, bidhaa, na ulipaji kodi.