Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, Awatakia Watumishi Heri ya Mfungo wa Ramadhani na Sikukuu ya Idd
28 Mar, 2025

Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, amewafuturisha watumishi wa Tume hiyo na kuwatakia heri ya Mfungo wa Ramadhani pamoja na sikukuu njema ya Idd. Hafla hiyo, iliyofanyika tarehe 27 Machi, 2025 jijini Dodoma, ililenga kudumisha mshikamano na mahusiano mazuri miongoni mwa watumishi.
Aidha, katika hafla hiyo, watumishi wa Tume wakiongozwa na Menejimenti walitumia fursa hiyo kumuaga Dkt. Nadhifa Kemikimba, ambaye alihudumu katika Tume katika Idara ya Maeneo Muhimu ya Kitaifa.