Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

Majaliwa akabidhi Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa Waziri wa Mipango kwa Mchakato wa Bunge
26 Mar, 2025
Majaliwa akabidhi Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa Waziri wa Mipango kwa Mchakato wa Bunge

Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ameongoza kikao cha tano cha Kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam leo Machi 1, 2025.

Katika kikao hicho, Mheshimiwa Majaliwa aliimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Kitila Mkumbo, Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili aipeleke kwenye Baraza la Mawaziri na hatimaye Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kutungiwa sheria.

Aidha, Kaimu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Mursali Milanzi, alianza kwa kudhibitisha muktasari wa kikao cha nne cha Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kilichofanyika Novemba 29, 2024. Alieleza hatua zilizotekelezwa tangu kikao hicho na umuhimu wa kuhakikisha mchakato wa kuandaa Dira hiyo unazingatia ushirikishwaji wa wadau na vipaumbele vya Taifa.

Hatua inayofuata ni kuwasilisha Rasimu kwa Baraza la Mawaziri na Bunge Kwenda kujadiliwa ili iweze kupitishwa rasmi na kuwa mwongozo wa maendeleo ya muda mrefu nchini.