Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Mipango Wajadili Utekelezaji wa Bajeti na Mpango wa Mwaka Ujao
26 Mar, 2025
Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Mipango Wajadili Utekelezaji wa Bajeti na Mpango wa Mwaka Ujao

Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Mipango limefanya kikao cha pili cha Baraza hilo tangu kuanzishwa kwake na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt. Fred Msemwa, ambaye ni Katibu Mtendaji wa Tume. Machi 20, 2025, Jijini Dodoma.

Mkutano huo, uliobeba kaulimbiu ya "Ushirikiswaji wa Watumishi katika kupanga na kutekeleza ni chachu ya ustawi wa Taasisi" ulihudhuriwa pia na wawakilishi kutoka TUGHE Taifa, Lengo kuu la kikao kilikuwa kujadili masuala muhimu yanayohusu Tume Pamoja na watumishi wake ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Msingi ya Tume kwa taifa. 

Miongoni mwa hoja zilizowasilishwa pamoja na kujadiliwa katika kikao hicho ni Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2024/25 pamoja na Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Tume kwa Mwaka 2025/26.