Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

MPANGO WA MAENDELEO 2027/28 KULENGA KUBADILI UKUAJI WA UCHUMI KUWA FURSA KWA WANANCHI
04 Nov, 2026
MPANGO WA MAENDELEO 2027/28 KULENGA KUBADILI UKUAJI WA UCHUMI KUWA FURSA KWA WANANCHI

MPANGO WA MAENDELEO 2027/28 KULENGA KUBADILI UKUAJI WA UCHUMI KUWA FURSA KWA WANANCHI

Serikali imeweka msukumo mpya katika uwekezaji wa sekta binafsi, ikilenga kukuza uchumi, kuongeza ajira na kuboresha maisha ya wananchi kupitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2027/28, utakaoendelea  kutekeleza Dira 2050.

Akiwasilisha mapendekezo ya Mpango huo leo Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), amesema uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.6 mwaka 2027, kutoka asilimia 5.9 mwaka 2025, huku ajira mpya zikitarajiwa kufikia wastani wa milioni 1.7, kutoka 981,000 mwaka 2025.

Aidha, amesema kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2026/27, miradi 243 yenye thamani ya dola bilioni 3.44 ilisajiliwa, ambapo asilimia 57.2 ya miradi hiyo ikiwa ya sekta ya viwanda.

Akizungumzia miezi mitatu Prof. Mkumbo amesema hatua hizo zimetoa matumaini kuwa malengo ya Taifa yanawezekana na kwamba ukuaji wa uchumi unaotarajiwa kufikia asilimia 6.6 mwaka 2027, huku  mfumuko wa bei ukitarajiwa kubaki chini ya asilimia tano.

Mhe. Mkumbo amesema kuwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2027/28 utaangazia maeneo sita ya kipaumbele ikiwa ni pamoja na; Uchumi imara jumuishi na shindani, uwezo wa watu maendeleo ya jamii, uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu wa mabdadiliko ya tabia nchi, vichocheo vya maendeleo, kuimarisha utekelezaji wa sekta za mageuzi na kuimarisha misingi ya uendelevu wa Taifa. 

Akifafanua zaidi  kuhusu ugharamiaji wa Mpango huo, amesema utazingatia uwiano wa 30 kwa 70 kati ya sekta ya umma na sekta binafsi: “Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2027/28 unakadiriwa kugharimu shilingi trilioni 89.3, ambapo sekta binafsi inatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 62.3, sawa na takribani asilimia 70 ya fedha zinazohitajika.”

Utekelezaji wa mipango hiyo, utafuatiliwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa e-Delivery na mbinu ya Lab Delivery Approach, kufuatilia maendeleo ya miradi na kupima matokeo yake.