Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

TANZANIA KUWASILISHA RIPOTI YA NCHI UTEKELEZAJI WA AJENDA 2030 UMOJA WA MATAIFA
06 Aug, 2026
TANZANIA KUWASILISHA RIPOTI YA NCHI UTEKELEZAJI WA AJENDA 2030 UMOJA WA MATAIFA

New York-Marekani
Tanzania inatarajiwa kuwasilisha ripoti ya nchi kuhusu
utekelezaji wa Ajenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu Julai 14, 2026 Jijini New York nchini Marekani kwenye Jukwaa la Ngazi ya Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa litakaloanza vikao vyake kuanzia Julai 7-15, 2026, Jijini humo.


Ripoti hiyo yenye lengo la kuonesha hatua zilizofikiwa katika kutimiza Ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa, Mafanikio na mafunzo yaliyopatikana katika utekelezaji wa ajenda hiyo kwa upande wa Tanzania, itawasilishwa na Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.


Aidha, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. Tausi M. Kida ataongoza ujumbe wa Tanzania katika vikao mbalimbali vya kitaalamu vya Ngazi ya juu katika jukwaa hilo la Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja kufungua kikao cha pembeni kilichoandaliwa na nchi kwa kushirikiana na nchi wanachama wa umoja wa mataifa, pamoja na mashirika yake.


Kikao hicho cha pembeni, kinalenga kujadili kwa kina kuhusu kuongeza thamani kwenye uchumi wa buluu na kukuza viwanda kwa lengo la kuendelea kuimarisha uchumi jumuishi na ongezeko la ajira kwa vijana na kinatarajiwa kutanyika Julai 9,
2026.