Tume ya Mipango ya Taifa imeungana na wanawake wote duniani kusherehekea Siku ya Wanawake Machi 8, 2025
26 Mar, 2025

Machi 8, 2025, Tume ya Mipango ya Taifa imeungana na wanawake wote duniani kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, ambapo maadhimisho ya kitaifa yamefanyika Mkoani Arusha. Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanawake wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na taasisi zinazochini yake walikuwa miongoni mwa maelfu ya wanawake waliojitokeza katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya siku hiyo kwa mwaka 2025, ambayo ilibeba kaulimbiu isemayo: "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na
Uwezeshaji.