Tume ya Mipango Yajadili Modeli ya Uchumi Jumla na Mpango Elekezi wa Dira ya Taifa 2050 Dodoma, Machi 11, 2025

Ikiwa mchakato wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uko kwenye hatua za kiserikali, wataalamu kutoka sekta mbalimbali wamekutana na kufanya kikao kazi chenye lengo la kuendelea kuweka misingi thabiti ya maendeleo ya muda mrefu kwa kujadili Modeli ya Uchumi Jumla na Mpango Elekezi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kikao kazi hicho kimeandaliwa na kiliandaliwa na Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, kupitia Tume ya Taifa ya Mipango, abacho kimejadili mifumo ya uchumi na mikakati ya kufanikisha ukuaji endelevu wa taifa ikihusisha tathmini kuhusu;
i. Mwelekeo wa Tanzania kuelekea hadhi ya taifa la kipato cha kati cha juu (UMIC) na hatua zinazohitajika kufikia pato la wastani la kila mtu.
ii. Viwango vya ukuaji wa uchumi (GDP) na mikakati ya kuhakikisha Dira ya Taifa 2050 inatekelezeka.
iii. Sekta muhimu zitakazochochea mageuzi ya kiuchumi na kuchangia malengo ya muda mrefu.