Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Mipango

TUME YA TAIFA YA MIPANGO YAJADILI MIKAKATI UTEKELEZAJI DIRA 2050
06 Aug, 2026
TUME YA TAIFA YA MIPANGO YAJADILI MIKAKATI UTEKELEZAJI DIRA 2050

Kuelekea Julai 1, 2026 ambapo Tanzania inaanza rasmi safari ya utekelezaji wa Dira 2050, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amekutana na watumishi wa Tume hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kuweka sawa mikakati ya mwisho kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa Dira hiyo. 

Katika kikao hicho, Dkt. Kida aliwaongoza watumishi hao kuhakiki hatua mbalimbali za maandalizi zilizofikiwa kuelekea uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 unaotarajiwa kufanyika Juni 29, 2026 jijini Dar es Salaam. 
Tume hiyo tayari imekamilisha nyenzo zote muhimu za utekelezaji wa Dira 2050, zikiwemo:

1.    Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu 2026/27-2050/51

2.    Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2026/27-2030/31

3.    Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2026/27. 

Aidha, Tume hiyo imekamilisha Mfumo wa kidijitali wa e-delivery utakaosimamia miradi ya maendeleo.