Wadau wa Kilimo Wajadili Ushiriki wa Sekta Katika DIRA 2050 Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC) anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji, Dkt. Blandina Kilama, ameongoza Kongamano lilihusisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo kwa lengo la kujadili nafasi ya kilimo katika utekelezaji wa DIRA 2050. Kongamano hilo limefanyika leo (tarehe 5 Agosti 2025) katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane, jijini Dodoma.
Kongamano hilo liliangazia fursa na changamoto zilizopo ndani ya Sekta ya Kilimo, ambapo wadau kutoka sekta ya umma, binafsi, taasisi za utafiti na elimu, pamoja na wakulima, walijadiliana kuhusu njia za kuongeza tija na ushindani katika Sekta ya Kilimo
Katika Kongamano hilo, Dkt. Kilama alisisitiza kuwa kilimo ni nguzo muhimu ya uchumi wa Taifa na kina nafasi ya kipekee katika kufanikisha utekelezaji wa DIRA 2050.
Kongamano hilo pia lilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Steven Nindi, aliyemwakilisha Katibu Mkuu, Bw. Gerald Mweli, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.
Viongozi hao waliunga mkono juhudi za NPC kwa kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote katika mageuzi ya sekta ya kilimo katika kutekeleza DIRA 2050.