Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida, amesema vijana ni nguvu kazi muhimu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akiwataka kutumia ubunifu, teknolojia, utafiti na ujasiriamali kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango anayeshughulikia Biashara na Ubunifu, Dkt. Blandina Kilama, amesema tafiti zenye shaidi na ubunifu ni njia bora ya kuleta suluhisho la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuchochea maendeleo katika utekelezaji wa Dira 2050.
Tume ya Taifa ya Mipango imetoa wito kwa Wakurugenzi wa Sera na Mipango kutoka wizara na taasisi mbalimbali kuongeza kasi ya kusajili miradi kwenye Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Mipango na Miradi ya Maendeleo wa e -Delivery ili kuharakisha utekelezaji wa Dira 2050
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Kinyasi Millya (Mb.) (wa nne kutoka kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida (wa tatu kutoka kushoto), na Bw. Shigeki Komatsubara, Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania (wa nne kutoka kulia), pamoja na viongozi mbalimbali na wadau wa maendeleo, wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu Tanzania, leo Agosti 31, 2026, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida, akizungumza na Bi. Akoth O. Kidew (miaka 11), Mwanzilishi na Kiongozi Mkuu wa Shirika la Small Hands, Big Change, mara baada ya ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu Tanzania 2026, inayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 04 Septemba 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, amesema Serikali inalenga kuhakikisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania unaendana na ongezeko la ajira na kipato kwa wananchi, akibainisha kuwa azma hiyo ni sehemu ya juhudi za kujenga uchumi jumuishi unaowanufaisha Watanzania. Mhe. Mkumbo ameyasema hayo, Agosti 31, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Wiki ya Ubunifu Tanzania 2026, iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Tume ya Taifa ya Mipango, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na wadau mbalimbali.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi M. Kida, leo Agost 20, 2026 amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Bw. Eliakimu Maswi, kuhusu ufungamanishaji wa Ajenda ya Kitaifa ya Mageuzi ya Kijamii na Maendeleo ya Mtaji Watu katika Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Dira 2050.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi M. Kida, akiwasilisha taarifa kuhusu mikakati ya kuhakikisha sera, sheria na kanuni zinaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Bungeni jijini Dodoma, Agosti 17, 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi M. Kida, amesema ushirikiano kati ya Serikali, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania na wadau mbalimbali ni muhimu katika kugeuza ubunifu, teknolojia na utafiti kuwa chachu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Unaweza kujisajili sasa kupitia https://summitpoint.co.tz/events/iwtz-2026
Tume ya Taifa ya Mipango imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 yanayoendelea jijini Tanga yakiongozwa na kauli mbiu imesemayo “Elimu, Ujuzi na Ubunifu njia ya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”.